About the poem: This is a contemporary, dramatized verse composed in Swahili for theatre arts performances. The poem mirrors the current situation in our country and the remedies that are to be implemented. The poem has 3 characters that represent different teams that seek common ground on issues that impact all of them.
Theme: High cost of living and contemporary societal issues
Tushangilie kenya taifa letu tukufu,
Kenya tunayoipenda daima,
Kenya nchi tunayoipenda daima.
WANABIASHARA: Solidarity forever, solidarity forever, solidarity forever for the
Makes us strong
KRA: Waah! Waah! Waah!
Humu sokoni mna nini?
WANABIASHARA: Humu sokoni mna ushuru
Ushuru ghali unaotuhujumu
Tunakosa kujikimu mnatudhulumu kiuchumi
Kwa yangu hamsini, kumi yake ni ushuru
Kwa yangu mia moja, ishirini yake ni ushuru
Kwa yangu mia mbili, sitini yake ni ushuru
Hamuoni mnatuhujumu?
KRA: Tulia ewe mpumbavu,
Hapa napo nipo kazini, sihitaji maziara kazini
Lipeni ushuru wenu na mapema, seriakli yako ikusaidie na mapema
Kuisajili vya kuisali vya mungu na view vya mungu
WANABIASHARA: Mahustler sisi ndio tuliowachagua,
Uhuru ghali ndio huu wameuchagua,
Mayooh!
Jameni?
(song) sina makosa wee bwana, mwataka kuniua bure bwana
KRA: Gazetini na mfike, tangazeni ushuru uko juu
Redioni na mfike, tangazeni ushuru uko juu
Runingani na mfike, tangazeni ushuru uko juu
WANABIASHARA: Redioni tumefika, malalamishi tumelete!
Mombasa adi Nairobi ushuru unatisha
Karo adi nauli, ushuru unaliza
Mama mboga na wachuuzi wote wanalizwa
Serikali inatuumiza, ushuru wakiupandisha
KRA: Mahustler wamewaskiza, matokeo mtayapata
Na mrejee kazini, ushuru wenu twaungoja
SERIKALI Hujambo mwananchi, karibu kwa yanayotendeka
Leo tumewaandalia Makala maalum,
Kuhusu ushuru unazidi kupandishwa!
Vita vilivyo Urusi, vinatisha
Vinachangia uhaba wa mafuta na vyakula
Upungufu wa madini na biashara ya duniya
Tulipe ushuru tuiokoe nchi na uchumi wetuu
WANANCHI: Mamayoooo!
Salaam maria umejaa neema,
Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko
Wanawake woote na yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa
Maria mtakatifu mama wa mungu
Tuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufe kwetu, Aaamiina
SERIKALI NA KRA: Maria mama wa mungu
Awaombee nyinyi wakosefu
Sasa na saa ya kazi zenu, ili muweze
Kulipa ushuru wenu
WANANCHI: Basi leo tumegoma ushuru huo mtaukoma
Kipato chetu mwatupokonya, nguvu zetu mwazinyonya
Basi leo tumewaonya, huu upuzi mtaukoma
Sisi leo, hatupangwingwi!
KRA: Basi leo natuungane, uovu huu na tuukomeshe
Ushuru na upunguzwe, sokoni na kuundwe
WANANCHI: Sokoni na kusinukee
SERIKALI: Wawawawawa!
Sisi ndio serikali!
Serikali yenye kemikali, kemikali zenye makali
Ruzuku na tunaziondoa, ushuru kuupandisha
KRA: Punguzeni hata kidogo
Wananchi mnawaumiza, polepole mnawauwa
Mzigo wenu na muuchukuwe, madeni zenu msitupimie
WANANCHI: Na kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe,
Na kila mtu atatoa Habari zake mwenyewe mbele ya mungu siku hiyo
inakuujaa
Leo ni leo tutaamua, serikali ni sisi tuliichagua
Ushuru ni wetu kuamua, uamuzi ni wetu kuufanya
SERIKALI: Tulieni basi tumewaskiza, ushuru huo tuwangalieni
Mapema kesho tutawaambieni, kuhusa hatima tumeiyafika
KRA & WANANCHI: Wakati ni sasa, kama sio sasa ni sasa hivi
Ujumbe twaungoja, kazi nazo zatungoja
SERIKALI: Basi uamuzi tumeuafika,kodi tumeipunguza
Ruzuku tumeirudisha,bei ya unga kuishusha
Gharama ya Maisha imeshuka, ushuru wenu nao umepunguka
Basi na mrejee kazini , mmeona mahustler wapo kazin.
KRA: Hujambo msikilizaji karibu kwa Habari za hivi punde
Ushuru umeshushwa, adi asilimia kumi na nne
WANANCHI NA KRA: Ha! Ha !ha, mlijifanya nyie wadwazi
Kumbe sisi ndio kuamua ushuru wetu umeshushwa, kazini tumerejea
Kuujenga wetu uchumi, na riziki kujitetea
WOTE: Kumi yako
Ishirini yako
Thelatini yenu , wote ni ushuru wetu
Pamoja tushikane mikono kuijenga nchi yetu
Tudumishe amani ,upendo na umoja
Kenya ni inchi yetu.
WOTE: Tumekomboa kenya taifa letu tukufu tumebadili mwendo daima, tutalinda katiba mpya, daima.
Anayependa kenya ni yule mwenye kutenda haki kwa watu wote daima.
Wenyenchi, Kenya kipenzi chetu hatutaiacha milele daima*2
Vuuuuuuu!!! Wana elite tumekafunga.
Mr. Nyangoga is a thespian who has always scripted plays, poems and traditional folk songs from learning situations looming in the society. He is a certified theatre arts director.